![]() |
Wanachama wa vuguvugu la Bring Back Our Girls waliandamana mjini Lagos Jumatano kutetea kuachiliwa kwa wasichana hao |
Ni wasichana 15 wanaoonekana kwenye kanda hiyo ya video ambayo inaaminika ilipigwa Siku ya Krismasi.
Video hiyo imepeperushwa hewani na shirika la utangazaji la marekani la CNN.
Maafisa wa Nigeria wamesema mashauriano kati ya serikali na wapiganaji hao wa Kiislamu yanaendelea lakini yatasalia kuwa siri kwa sababu za kiusalama na ili kuzuia wanaofanikisha wazungumzo hayo wasitambulike.
![]() |
Mamake mmoja wa wasichana waliotekwa |
Kanda hiyo ya video ndiyo ya kwanza kutolewa ikiwaonesha wasichana hao tangu mwezi Mei mwaka 2014.
Serikali ya Nigeria imekosolewa kwa kushindwa kuwakomboa wasichana hao.
Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama ni mmoja wa watu mashuhuri walioshiriki katika kampeni ya kupigania kukombolewa kwa wasichana hao.
0 comments:
Post a Comment