![]() |
|
![]() |
''Tuliwapoteza wenzetu wengi,,,,,wengi sana,, sijui hata ni wangapi waliojeruhiwa'' alisema mwanajeshi huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake |
Hata hivyo mwanajeshi huyo anasema kuwa idadi ya wapiganaji hao ilikuwa kubwa mno hata wanajeshi kadhaa walitoroka ilikuokoa maisha yao.
''Walikuwa na silaha nzito nzito na kali kuliko zetu'' afisa huyo aliiambia idhaa ya BBC Hausa.
![]() |
Mwanajeshi mmoja aliyeko Borno ameielezea BBC kuwa''wapiganaji wa Boko Haram waliwavizia na kuwashambulia alfajiri na mapema wakiwa wamelala.'' |
''Baadhi yetu walitoroka maji yalipozidi unga''
''Tuligundua idadi ya wavamizi ilikuwa ni kubwa kuliko yetu'' mwanajeshi mwengine aliiambia shirika la habari la AFP.
Hata hivyo jeshi lilijitahidi na kuikomboa kambi hiyo baada ya mashambulizi ya angani kuwasili na kuwaokoa wanajeshi walikuwa wamesakamwa ardhini.
Idadi kamili ya waliouawa haijajulikana.
0 comments:
Post a Comment