mazingira
michezo
ujasiriamali
dira ya dunia
siasa
waasi
ict master
program zote
tekinologia
mazingira
elim
boko haram
habari
alshababu
kimataifa
kitaifa
burundi
rwanda
alshababu
video
Friday, April 8, 2016
Papa Francis kutoa tamko muhimu kuhusu ndoa
By
Suxiya Chinese language center
on 6:06:00 AM
Image copyright
AFP
Image caption
Papa Francis amekuwa akitofautiana na wahafidhina kanisa Katoliki
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo anatarajiwa kutangaza wazi msimamo wake kuhusu ndoa, njia za kupanga uzazi na malezi ya watoto.
Tangazo hilo linatarajiwa kuwa kwenye ripoti ya mikutano miwili mikuu ya kutoa maamuzi kuhusu sera za kanisa hilo, maarufu kama sinodi.
Wengi wanatumai kwamba ripoti hiyo itafungua njia kwa kanisa hilo kutoa sakramenti ya komunyo kwa watu waliopewa talaka na wale waliooa tena, jambo ambalo wahafidhina katika kanisa hilo wamekuwa wakipinga.
Ripoti hiyo ni matokeo ya kazi aliyoifanya Papa huyo kwa miaka mitatu.
Mwandishi wa BBC anayeangazia masuala ya kidini Caroline Wyatt anasema ripoti hiyo ambayo kwa Kiingereza hujulikana kama Apostolic Exhortation (Ujumbe wa Papa kwa Waumini) ni nyaraka yenye zaidi ya kurasa 200.
Ripoti hiyo ya sasa imepewa kichwa The Joy of Love (Furaha ya Upendo).
Image copyright
EPA
Image caption
Papa Francis alituma hojaji kwa watu nchi mbalimbali duniani kuomba maoni
Papa Francis alituma hojaji kwa familia maeneo mbalimbali ya dunia akiwaomba wamjulishe matumaini yao na wasiwasi wao.
Baadaye, aliwaita maaskofu na makadinali kwa mikutano miwili ya sera za kanisa mjini Roma.
Kwenye mkutano huo, aliwahimiza kujadiliana na hata kutofautiana kuhusu masuala ambayo hugawanya waumini wa kanisa hilo katika nchi nyingi.
Masuala hayo ni pamoja na kutoa komunyo kwa watu waliopewa talaka na wale walioolewa tena, njia za kupanga uzazi na pia Wakatoliki ambao ni wapenzi wa jinsia moja.
Mwandishi wetu anasema ripoti hiyo itaonyesha wazi msimamo wa Papa Francis.
Baadhi tayari wanasema itashangaza wengi, huku Papa akijitosa katika bahari ya mafundisho ya kanisa Katoliki kuhusu familia.
Wahafidhina hawamtaki abadilishe imani na msimamo wa kanisa, lakini watu wenye msimamo huru wanatumai kwamba ataliambia kanisa liwe na huruma na kuwakumbatia wale watu walio kwenye familia wasiokumbatia kikamilifu mafundisho ya kanisa.
Baba Mtakatifu aosha miguu ya waislamu
Papa: Uoga utawafanya Wakristo wafungwa
Papa Francis aingia Instagram
Baadhi katika kanisa Katoliki wametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za kumruhusu padri au askofu kuamua faraghani kwa kuzingatia uzito wa kila kisa, iwapo Mkristo aliyepewa au kupeana talaka na kuoa au kuolewa tena anaweza kukumbatiwa kwenye kanisa na kuruhusiwa kupokea komunyo.
Image copyright
AP
Image caption
Papa Francis ameifanyia kazi ripoti hiyo kwa miaka mitatu
Ingawa wale wanaotaka kanisa likumbatie mambo ya kisasa kama vile Kadinali Walter Kasper wa Ujerumani wanaunga mkono sera hii, wahafidhina wanasisitiza kwamba itadunisha uzito wa msingi uliowekwa na Yesu kwamba ndoa haiwezi ikavunjwa.
Wakati wa kumalizika kwa sinodi ya mwaka jana, Papa Francis aliwakosoa viongozi wa kanisa aliosema wamelifumbia macho suala hilo na kusema kwamba kuendelea kusisitiza kuheshimiwa kwa mafundisho ya dini kikamilifu ni kukosa kutilia maanani dhiki wanayopitia watu wengine katika familia.
Kwa Picha: Maisha ya Papa Francis
Nyaraka hiyo ya papa inatarajiwa kutoa wito wa kuwepo kwa maandalizi mema zaidi kabla ya ndoa na pia kusisitiza mtazamo wa sinodi kwamba ndoa za wapenzi wa jinsia moja haziwezi zikawekwa kwenye kiwango sawa na ndoa za watu wa jinsia tofauti.
Newer Post
Older Post
0 comments:
Post a Comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
uundaji wa roboti
Roboti ni mashine inayotekeleza shughuli peke yake bila kuendeshwa na binadamu . Kuna tofauti kati ya nchi na nchi kuhusu kiwango na ugumu...
Video ya Boko Haram yaonesha wasichana wa Chibok
Wanachama wa vuguvugu la Bring Back Our Girls waliandamana mjini L...
Tanzania: Simba yachinjwa kombe la Shirikisho
...
Well come in talanta group olasity Kati arusha Tanzania we produce good instruments for water management like ports. Tank ect
tok kwa maelezo piga sm 0759894855
Watano kuwania tuzo ya mwanasoka bora Afrika 2015
Wagombea watano wa tuzo ya BBC kwa mwanasoka bora wa mwaka 2015 wametangazwa kwenye hafla maalum iliyoandaliwa mjini Johannesburg, Afri...
The best hidden features in Windows 10's major update
Share on Facebook (2,710) Tweet Share Pin Microso...
UMUHIMU WA KUTUNZA KUMBUKUMBU ZA BIASHAURA
Tunzaji wa kumbukumbu za biashara yako ni muhimu sana kwani mali bila daftari basi hupotea bila habari ...
aina za robot
Leo robots ni kutumika katika kila uga: sekta ya viwanda, jeshi, nafasi ya utafutaji, usafirishaji na matumizi ya tiba. Ni kwa saba...
FIFA yatishia kuipiga marufuku Nigeria
Shirikisho la kandanda duniani limetishia kuipiga marufuku Nigeria kutoka kwenye mashindano yeyote ya kimataifa iwapo haitamrejesha afi...
Jino kubwa la nyangumi lapatikana Australia
Jino hilo lilipatikana mwezi Februari Jino kubwa la nyangumi limepatikana ufukweni Australia, na kuwa thibitisho la ...
Follow Us on Facebook
Blog Archive
►
2017
(3)
►
May
(3)
▼
2016
(86)
►
June
(2)
►
May
(26)
▼
April
(50)
DIRA YA DUNIA ALHAMISI 28.04.2016
dira dunia
yemi amegusa wangapi ?
je ya linex imekugusa?
Wenger:Arsenal ilipoteza taji la ligi nyumbani
Trump achekwa kwa alivyotamka Tanzania
Magufuli: Polisi sharti wajirekebishe
Mazungumzo ya amani ya Burundi yaahirishwa
Raia wa Burundi waendelea kulitoroka taifa lao
Benki ya Chase yafunguliwa tena Kenya
Dola milioni 800 za IS zaharibiwa na Marekani
Rwanda yawaondosha raia wake Zambia
nyangumi aonekana pembezoni mwa fukwe za coco bichi
Jino kubwa la nyangumi lapatikana Australia
Al-Shabab aliyejiunga na IS anaswa Somalia
Salamu TMK - Mfuko Official Video
Atolewa kwenye ndege kwa kuongea Kiarabu
Raia waliolazimika kutoka nje ya mahakama baada ...
Machar afuta mpango wa kurejea Juba
Filamu nyingine ya Avatar kuongezwa
Boko Haram wavamia kambi ya jeshi Nigeria
Korea Kaskazini kulipua bomu la nyuklia
UN: Burundi inawatesa wapinzani wake
Mkuu wa shirika la UN amshutumu Trump
Tetemeko la pili laikumba Kumamoto, Japan
Sudan Kusini yajiunga na Afrika Mashariki
''Karibu niwe mlipuaji wa kujitoa mhanga''
Video ya Boko Haram yaonesha wasichana wa Chibok
...
Video; ERICK OMMONDI
UMUHIMU WA KUTUNZA KUMBUKUMBU ZA BIASHAURA
utunzaji wa kumbukumbu
Ndege za Marekani zaua al shabab Somalia
Mulipuko wa homa ya manjano DRC
Roboti kuchukua kazi za raia Australia
aina za robot
FIFA yatishia kuipiga marufuku Nigeria
Tanzania: Simba yachinjwa kombe la Shirikisho
UEFA: Man City kuikabili PSG
Watu 5 wauawa Ruyigi Burundi
uundaji wa roboti
Papa Francis kutoa tamko muhimu kuhusu ndoa
Tanzania na Rwanda zafungua ukurasa mpya
Mamba mkubwa auawa Florida
Ted Cruz amshinda Trump mchujo Wisconsin
US na China kushirikiana dhidi ya Korea Kaskazini
The History of Computers
history of sd card
Secure Digital
contact us facebook phone no
►
March
(8)
►
2015
(22)
►
December
(8)
►
November
(14)
Followers
Copyright © 2012 News Magazine Theme. Designed by
Templateism
0 comments:
Post a Comment