Ungana nami
katika kukuletea makala hii muhimu, naamini itakua na mchango mkubwa kwako
mjasiriamali na mfanyabiashara, pia hata kwa yule ambaye ana lengo ama wazo la
kuwa na biashara siku za usoni.
Aina ya vitabu ama kumbukumbu ambazo mfanyaabiashara anatakiwa kuwa
nazo.
No1. Kumbukumbu
zinazohusu manunuzi / purchases
No.2
Kumbukumbu zinazohusu mauzo/ sales
No.3
Kumbukumbu gharama za uendeshaji/ operating expenses
No. 4
Kumbukumbu zinazohusu gaharama za usimamizi wa biashara/ administrative
expenses
Kwanini kuwa na kumbukumbu hizi ni muhimu?
Kuandaa na
kuwa na kumbukumbu hizi kuhusu biashara yako ni muhimu kwani zitakusaidia
katika mambo yafuatayo;
·
Kujua faida halisi inayopatikana
katika biashara yako.
·
Kujua kwa uhalisia kiwango cha kodi
utakachotozwa kulingana na kiasi cha faida iliyopatikana
·
Kufanya tathimini ya biashara yako
kwa urahisi endapo inakua ama inahitaji kuboreshwa zaidi.
· Kuharakisha upatikanaji wa mkopo hasa
kutoka mabenki.
· Kusaidia kupanga bei itakayoendana na
nguvu ya ushindani na kiasi cha faida unachohitaji kukipata.
Hivyo, kama
tulivyokwishaona uaandaaji na utunzaji kumbukumbu ni muhimu sana hususani
katika ukuaji na maendeleo ya biashara yako. Tukumbuke msemo usemao mali
bila daftari hukwisha bila habari.
Unawezaje kuandaa vitabu vya biashara yako?
Katika sehemu
hii tutaanza kujifunza namna na umuhimu wa kuandaa vitabu ama kumbukumbu
zihusuzo biashara yako kama ifuatavyo;
No.1 Kumbukumbu
(vitabu) zinazohusu manunuzi
Hizi ni
taarifa ambazo zinakusaidia mfanyabiashara kujua kiasi cha manunuzi uliofanya na thamani yake. Kuwepo kwa taarifa
hizi kunasaidia mfanyabiashara kupanga bei mathalani atakuwa anafahamu ni bei
gani alio nunulia kwa kila bidhaa alio nayo.
Mara nyingi taarifa hizi hutokana na jumla ya
risit za manunuzi unazopokea unaponunua bidhaa zako kwa jumla ama rejareja.
Lakini pia ni muhimu kurekodi taarifa hizo za manunuzi katika daftari ama
kitabu cha manunuzi katika mpangilio mzuri kufuatana na tarehe.
Upangaji huu
ni muhimu kwani utakusadia kujua lini na kiasi gani cha bidhaa ulinunua na
zenye kugharimu kiasi gani. Lakini pia itakusadia sana katika ulipaji wa kodi
ya ongezeko la thamani (VAT) endapo biashara yako imeandikishwa katika kulipa
VAT.
Hatua katika
uandaaji.
I. Kusanya risiti zako zote za manunuzi
ya bidhaa.
II. Orodhesha/rekodi taarifa hizo katika
daftari maalumu kwa kufuata tarehe. Muonekano wake utakua kama ufuatao apa
chini;
Tarehe
|
Bidhaa
|
Kiasi
|
Gharama
|
10/11/2013
|
mchele
|
Kg 10
|
15,000/-
|
12/11/2013
|
Mafuta ya kula
|
Lita 20
|
30,000/-
|
III.
Kutegemea na muda uliojipangia
unaweza kujua ni kiasi gani cha manunuzi umefanya ikiwa ni kwa wiki mwezi ama
mwaka.
No.2
Kumbukumbu (vitabu) zinazohusu mauzo
Hizi ni
taarifa ambazo zinakusaidia mfanyabiashara kujua kiasi cha mauzo uliofanya na thamani yake. Kuwepo kwa taarifa
hizi kunasaidia mfanyabiashara kujua
kiwango cha uhitaji wa wateja katika kila bidhaa, kutegemea kasi ya
wateja katika kuinununua; inasaidia kujua ni bidhaa ipi inauzika zaidi
ukilinganisha na nyingine.
Pia huweza
kujua kiwango cha faida ghafi(gross profit) kutoka katika kila bidhaa
iliyouzwa.
Mara nyingi taarifa hizi hutokana na rekodi za
mauzo uliyofanya endapo ni kwa siku, wiki, mwezi ama mwaka. Lakini pia ni
muhimu kurekodi taarifa hizo za mauzo katika daftari ama kitabu cha mauzo
katika mpangilio mzuri kufuatana na tarehe.
Upangaji huu
ni muhimu kwani utakusadia kujua lini na kiasi gani cha bidhaa uliuza na
zina thamani ya kiasi gani. Lakini pia
itakusadia sana katika ulipaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) endapo
biashara yako imeandikishwa katika kulipa VAT.
Hatua katika uandaaji.
I. Kuwa na utaratibu wa kutunza kopi ya
risiti kila unapotoa risit kwa mteja.
(ikiwa
huna basi orodhesha kumbukumbuzako za mauzo, kwa kila bidhaa kufuatana na hatua
ya (ii) apa chini
II. Orodhesha/rekodi taarifa hizo katika
daftari maalumu kwa kufuata tarehe. Muonekano wake utakua kama ufuatao apa
chini;
Tarehe
|
Bidhaa
|
Kiasi
|
Gharama
|
10/11/2013
|
mchele
|
Kg 3
|
8,000/-
|
12/11/2013
|
Mafuta ya kula
|
Lita 6
|
3,000/-
|
III.
Kutegemea na muda uliojipangia
unaweza kujua ni kiasi gani cha mauzo umefanya ikiwa ni kwa wiki mwezi ama
mwaka.
Katika sehemu
ya inayofuata ya makala hii tutaangalia
namna ya kuandaa na kumbukumbu zihusuzo gharama zihusuzo uendeshaji na
usimamizi wa biashara yako, endelea
kufuatilia makala hii kwa manufaa yako mjasiriamali na ukuaji wa biashara
yako.....
0 comments:
Post a Comment