![]() |
Wateja wanaruhusiwa kutoa hadi $10,000 |
Wateja ambao walikuwa wameweka pesa zao katika benki hiyo wanaruhusiwa kutoa hadi shilingi 1milioni ($10,000; $6,800).
Benki ya Chase ndiyo ya tatu kuwekwa chini ya mrasimu nchini Kenya katika kipindi cha miezi sita, hatua iliyozua wasiwasi kuhusu uthabiti wa sekta ya benki nchini Kenya.
- Benki ya Chase ilivyovuma kisha ikayumba Kenya
- Video: Wateja wa Chase Bank wafurahia kufunguliwa kwake
Gavana wa Benki Kuu ya Kenya (CBK) Dkt Patrick Njoroge amepuuzilia mbali wasiwasi kuhusu sekta hiyo na kusema benki hiyo inachukua hatua kudhibiti hali.

Benki ya Chase itasimamiwa kwa muda na Benki ya Kenya Commercial (KCB).
Afisa mkuu mtendaji wa KCB Joshua Oigara ameeleza matumaini yake kwamba benki hiyo itajikwamua na kuimarika tena.
0 comments:
Post a Comment