![]() |
Trump alishambulia sana sera ya kigeni ya Obama |
Mgombea urais wa
chama cha Republican Donald Trump amekejeliwa mtandaoni baada ya
kuonekana akiboronga akitamka Tanzania wakati wa kutoa hotuba.
Bw
Trump alikuwa akizungumzia mashambulio ya kigaidi yaliyotekelezwa katika
mabalozi ya Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 wakati wa
kuzungumzia sera yake ya kigeni.Badala ya kutamka vyema ‘Tanzania’ anasikika akitamka ‘Tan-zay-nia’.
Mashambulio hayo yalitekelezwa na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda.
Msemaji wa ikulu ya White House pia alimcheka Bw Trump alipoulizwa kuhusu vile mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York alivyotamka jina Tanzania.
“Kweli, yamkini jinsi ya kutamka huwa haijaelezwa kwenye kifaa cha kuonesha maandishi ya hotuba,” alieleza afisa wa habari wa ikulu Bw Josh Earnest.
0 comments:
Post a Comment