![]() |
Trump mwishoni mwa mwaka jana alipendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani |
Mkuu wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Haki za Kibinadamu ameshutumu sera za
mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani, akisema ni sawa
na ushenzi.
Zeid Raad al-Hussein, ingawa hakumtaja Bw Trump moja
kwa moja, alizungumzia hatua ya mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New
York kuunga mkono mateso pamoja na sera zake kali dhidi ya Waislamu.“Ushenzi na ulokole si thibitisho la uongozi thabiti,” Hussein alisema.
Kamishna huyo pia amekosoa mpango wa mgombea mwengine Ted Cruz wa kuweka mpango wa kupeleleza maeneo wanamoishi Waislamu.
“Kutoa matamshi ya chuki, kuchochea na kuwatenga wengine si jambo la kuburudisha watu nalo, au jambo la kujifaidi kisiasa,” Bw Hussein ameambia hadhira katika mji wa Cleveland, Ohio.
Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislam
Vigogo wa chama
cha Republican nchini Marekani wamemkemea mwenzao Donald Trump,
anayetaka kuwania urais kupitia chama hicho, kwa kupendekeza Waislamu
wazuiwe kuingia Marekani.
Mmoja wa wanaoshindani tiketi ya kuwania
urais Jeb Bush amesema Bw Trump "mwenye kasoro akilini”. Makamu wa rais
wa zamani Dick Cheney naye alisema pendekezo hilo "linaenda kinyume na
yote ambayo huwa tunatetea”.Ikulu ya White House, Umoja wa Mataifa na viongozi wa Kiislamu pia wamekosoa matamshi hayo ya Trump.
Bw Trump alikuwa amesema Waislamu wengi wana "chuki” dhidi ya Marekani.
Kwenye hotuba wakati wa kampeni, aliomba "Waislamu wote wazuiwe kuingia Marekani hadi wawakilishi wa nchi wajue ni nini kinachoendelea”
Meneja wake wa kampeni alisema marfuku hiyo ingeathiri "kila mmoja” bila kubagua kama ni mhamiaji au mtalii.
- Mambo 20 makuu anayoamini Donald Trump
- Trump ashutumiwa kwa kupanga kufurusha wahamiaji
- Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na Saddam
Wiki iliyopita, wanandoa wawili Waislamu, ambao wanaaminika kukumbatia itikadi kali, walifyatua risasi na kuwaua watu 14 na kuwajeruhi wengine 21 katika kituo cha afya San Bernardino, jimbo la California.
Bw Trump alishangiliwa sana aliporudia ahadi yake katika mkutano wa kampeni jimbo la South Carolina saa chache baada ya kutoa matamshi hayo mara ya kwanza.
Ameongeza: "Mmoja wa wagombea wanaoongoza katika kinyang’anyiro cha kutaka kuwa rais wa nchi hii alitangaza, miezi kadha iliyopita, kujitolea kwake kutumia mateso (…) kuumiza watu wengine, ili watoe habari au wabuni habari ambazo hawazo nazo.”
![]() |
Bw Hussein amesema si vyema kukiuka haki za wengine kujifaa kisiasa |
0 comments:
Post a Comment