Mkufunzi wa Arsenal
Arsene Wenger amesema kuwa timu yake ilipoteza harakati za kushinda
ligi wakati wa kucheza mechi za nyumbani dhidi ya timu zilizo chini ye
jedwali.
Arsenal iliopo katika nafasi ya nne imeshinda mechi sita kati ya mechi 16 ilizocheza.
Baadhi ya mashabiki wamemtaka raia huyo wa Ufaransa kuondoka katika mechi za hivi karibuni.
Ni lazima tujue kwamba ugenini tumekuwa washindi .
Arsenal
Lakini nyumbani dhidi ya timu ndogo tulipoteza pointi nyingi,alisema Wenger.
Maandamano zaidi yanatarajiwa wakati wa mechi ya Jumamosi katika uwanja wa Emirates dhidi ya Norwich.
Mgombea urais wa
chama cha Republican Donald Trump amekejeliwa mtandaoni baada ya
kuonekana akiboronga akitamka Tanzania wakati wa kutoa hotuba.
Bw
Trump alikuwa akizungumzia mashambulio ya kigaidi yaliyotekelezwa katika
mabalozi ya Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 wakati wa
kuzungumzia sera yake ya kigeni.
Badala ya kutamka vyema ‘Tanzania’ anasikika akitamka ‘Tan-zay-nia’.
Mashambulio hayo yalitekelezwa na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda.
Msemaji
wa ikulu ya White House pia alimcheka Bw Trump alipoulizwa kuhusu vile
mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York alivyotamka jina Tanzania.
“Kweli,
yamkini jinsi ya kutamka huwa haijaelezwa kwenye kifaa cha kuonesha
maandishi ya hotuba,” alieleza afisa wa habari wa ikulu Bw Josh Earnest.
Mwanafunzi wa chuo kikuu raia wa
Iraq katika jimbo la California nchini Marekani anasema kuwa alitolewa
kutoka kwenye ndege ya shirika la ndege la Southwest baada ya kufanya
mazungumzo kwa lugha ya kiarabu.
Shirika hilo la Southwest
lilisema kuwa Khairuldeen Makhzoomi aliondolewa ndegeni tarehe 9 mwezi
Aprili kabla ya ndege hiyo kupaa.
Bw Makhzoomi anasema alikuwa
akizungumza na mjomba wake kwa njia ya simu kuhusu hotuba ya katibu mkuu
wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Anasema kuwa mwanamke mmoja kwenye ndege hiyo alimkodolea macho wakati alitamka jina "Inshallah" akimaanisha Mungu akipenda.
Baada ya kutumia jina hili mfanyikazi wa shirika la Southwest alimsindikiza nje ya ndege.
Bw
Makhzoomi ambaye aliingia nchini Marekani kama mkimbizi kutoka Iraq na
sasa ni mwanafunzi wa chuo cha Carlifonia cha Berkeley, aliambiwa kuwa
hawezi kuingia tena kwenye ndege hiyo.
Serikali ya Sudan
Kusini imesema kuwa kiongozi wa waasi Riek Machar, amefutilia mbali
mpango wake wa kurejea Juba kwa muda usiojulikana.
Msemaji wa
serikali Michael Makuei amesema kuwa makamu wa bwana Machar, alitaka
kurejea Juba na silaha nzito nzito, zikiwemo, magari ya kivita,
makombora na bunduki nzito nzito.
Aidha amesema kuwa serikali ya
nchi hiyo tayari imeruhusu wanajeshi elfu moja mia tatu na sabini kati
ya elfu moja mia nne na kumi kurejea Juba kuja kumlinda Bwana Machar.
Amesema kuwa utawala wa nchi hiyo hautaruhsu wanajeshi zaidi kurejeshwa Juba, kutokana na sababu za kiusalama
Filamu ya kwanza ya Avatar ilitolewa 2009 na iliwashirikisha Sam Worthington na Zoe Saldana
Watengenezaji wa
filamu ya Avatar franchise wamesema kutatolewa filamu zaidi katika
mwendelezo huo wa filamu, filamu ijayo ikitarajiwa kutolewa 2018.
Mwelekezi wa filamu hizo James Cameron ametangaza kwamba filamu hizo zitaendelezwa hadi makala ya tano itakayotolewa 2023.
Alikuwa
tayari amethibitisha kwamba filamu tatu zaidi zingetolewa lakini
amefichua kwamba kuna mambo mengi sana ya kuelezwa kwenye hadithi hiyo
na makala zijazo tatu hazitoshi.
Kote duniani, Avatar inasalia kuwa filamu iliyofanikiwa zaidi katika historia.Filamu hiyo imezoa $2.7bn tangu kutolewa wake 2009.Filamu ijayo ya Avatar itatoka 2018, na hizo nyingine 2020, 2022 na 2023.
Trump mwishoni mwa mwaka jana alipendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani
Mkuu wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Haki za Kibinadamu ameshutumu sera za
mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani, akisema ni sawa
na ushenzi.
Zeid Raad al-Hussein, ingawa hakumtaja Bw Trump moja
kwa moja, alizungumzia hatua ya mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New
York kuunga mkono mateso pamoja na sera zake kali dhidi ya Waislamu.
“Ushenzi na ulokole si thibitisho la uongozi thabiti,” Hussein alisema.
Kamishna huyo pia amekosoa mpango wa mgombea mwengine Ted Cruz wa kuweka mpango wa kupeleleza maeneo wanamoishi Waislamu.
“Kutoa
matamshi ya chuki, kuchochea na kuwatenga wengine si jambo la
kuburudisha watu nalo, au jambo la kujifaidi kisiasa,” Bw Hussein
ameambia hadhira katika mji wa Cleveland, Ohio.
Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislam
Trump anaongoza kwenye kura za maoni miongoni mwa wagombea wa Republican
Vigogo wa chama
cha Republican nchini Marekani wamemkemea mwenzao Donald Trump,
anayetaka kuwania urais kupitia chama hicho, kwa kupendekeza Waislamu
wazuiwe kuingia Marekani.
Mmoja wa wanaoshindani tiketi ya kuwania
urais Jeb Bush amesema Bw Trump "mwenye kasoro akilini”. Makamu wa rais
wa zamani Dick Cheney naye alisema pendekezo hilo "linaenda kinyume na
yote ambayo huwa tunatetea”.
Ikulu ya White House, Umoja wa Mataifa na viongozi wa Kiislamu pia wamekosoa matamshi hayo ya Trump.
Bw Trump alikuwa amesema Waislamu wengi wana "chuki” dhidi ya Marekani.
Kwenye
hotuba wakati wa kampeni, aliomba "Waislamu wote wazuiwe kuingia
Marekani hadi wawakilishi wa nchi wajue ni nini kinachoendelea”
Meneja wake wa kampeni alisema marfuku hiyo ingeathiri "kila mmoja” bila kubagua kama ni mhamiaji au mtalii.
Lakini Bw Trump aliambia Fox News kwamba
haingeathiri “watu wanaoishi humu nchini (Marekani), akiongeza kuwa
Waislamu wanaohudumu katika jeshi la Marekani wangekaribishwa
"nyumbani”.
Matamshi hayo ya Bw Trump yalitolewa Marekani ikiendelea
kuomboleza kufuatia shambulio mbaya zaidi la kigaidi kutekelezwa tangu
shambulio la Septemba 11, 2001.
Wiki iliyopita, wanandoa wawili
Waislamu, ambao wanaaminika kukumbatia itikadi kali, walifyatua risasi
na kuwaua watu 14 na kuwajeruhi wengine 21 katika kituo cha afya San
Bernardino, jimbo la California.
Bw Trump alishangiliwa sana
aliporudia ahadi yake katika mkutano wa kampeni jimbo la South Carolina
saa chache baada ya kutoa matamshi hayo mara ya kwanza.
Ameongeza: "Mmoja wa wagombea wanaoongoza katika kinyang’anyiro cha
kutaka kuwa rais wa nchi hii alitangaza, miezi kadha iliyopita,
kujitolea kwake kutumia mateso (…) kuumiza watu wengine, ili watoe
habari au wabuni habari ambazo hawazo nazo.”
Bw Hussein amesema si vyema kukiuka haki za wengine kujifaa kisiasa
Wakati wa kampeni, bw Trump alisema kwamba mateso
wakati mwingine hufanikiwa na akaahidi kurejesha njia hatari zaidi
kuliko kutumia maji kulazimisha washukiwa kufichua habari.Njia hizo zilitumiwa na jeshi la Marekani katika washukiwa wa ugaidi lakini zilipigwa marufuku na utawala wa Bw Obama.
Tetemeko hilo lilisababisha kuporomoka kwa majengo
Maafisa nchini Japan wanasema kuwa tetemeko kubwa la ardhi limewaua takriban watu 19 na kusababisha uharibifu mkubwa.
Tatemeko
hilo ambalo ni la pili kukumba kisiwa cha Kyushu ndani ya siku mbili,
limesababisha kuporomoka kwa majengo, limeharibu barabara pamoja na
mifumo ya maji na umeme.
Tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 7.3 kwenye vipimo vya Richter.
Tetemeko
hilo la ardhi, ambalo chanzo chake ni kilomita 10 chini ya ardhi karibu
na mji wa Kumamoto, lilikuwa kubwa na liliathiri eneo kubwa kuliko la
kwanza lililotokea katika mji huo wa Kumamoto Alhamisi usiku.
Watu wengi wamejeruhiwa
Afisa wa serikali wa Kumamoto Tomoyuki Tanaka ameambia AP kwamba idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.
Wanajeshi 20,000 wametumwa kusaidia juhudi za uokoaji lakini jitihada za uokoaji zimetatizwa na mitetemeko mingine midogomidogo.
Waziri mkuu Shinzo Abe amekuwa na mipango ya kuzuru ki