1. Hazifanyi kazi hadi zichajiwe au ziunganishwe kwenye umeme.
2. Zinaweza kuzima ghafla na kukupotezea kazi ambayo hukuisevu.
3. Kompyuta humfanya mtu awe “addicted” kila muda ukiona kompyuta mikono inakuwasha.
4. Kompyuta hubadilika haraka kimatumizi na kiumbo. Kila siku zinatolewa aina mpya, hivyo utajikuta unatumia kompyuta ambayo ishapitwa na wakati.
5. Matatizo ya programu, programu huuzwa tofauti na kompyuta kwahiyo kila kitu unanunua hupewi pamoja na kompyuta.
6. Tatizo la vifaa, ni gharama sana kununua kifaa kama kimeharibika kwenye kompyuta yako.
7. Kompyuta huharibika haraka sana, inahitaji matunzo makubwa ili kuinusuru.
8. Virusi, kompyuta huhathiliwa sana na virusi na kukufanya uweze kupoteza nyaraka zako muhimu katika kompyuta.
9. Kompyuta huhitaji kubadilishwa mara kwa mara kwani kila siku zinatoka aina mpya. Hii itakusababisha kuingia gharama mara kwa mara.
10. Kompyuta huzidisha kazi kwani kama wewe ni mfanyakazi utahitajika ujibu “email” za bosi wako hata ukiwa nyumbani tofauti na zamani..
-
0 comments:
Post a Comment