Kuna utata kuhusu ni nani alimuokoa na jina la msichana ni lipi. |
Kumezuka utata
kuhusu msichana wa Chibok ambaye aliokolewa nchini Nigeria. Kwanza jeshi
linasema kuwa ndilo lilimuokoa msichana huyo aliyetjwa jina kuwa
Falmata Mbalala.
Hata hivyo wanaharakati na viongozi wa kijamii
wanasema kuwa msichana aliyeokolewa, jina lake ni Amina Ali Nkek na kuwa
alipatikana katika msitu wa Sambisa na kundi la vijana na kudumisha
usalama.Msitu huo ndio maficho makuu ya wanamgambo wa Boko Haram.
Mwenyeki wa chama cha wazazi wa Cibok mjini Abuja Hosea Abana Tsambido aliiambia BBC kuwa vijana hao walikuwa na habati kubwa kumpata msichana huyo.
0 comments:
Post a Comment