Friday, April 29, 2016

Wenger:Arsenal ilipoteza taji la ligi nyumbani

Arsene Wenger
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa timu yake ilipoteza harakati za kushinda ligi wakati wa kucheza mechi za nyumbani dhidi ya timu zilizo chini ye jedwali.
Arsenal iliopo katika nafasi ya nne imeshinda mechi sita kati ya mechi 16 ilizocheza.
Baadhi ya mashabiki wamemtaka raia huyo wa Ufaransa kuondoka katika mechi za hivi karibuni.
Ni lazima tujue kwamba ugenini tumekuwa washindi .
 Arsenal
Lakini nyumbani dhidi ya timu ndogo tulipoteza pointi nyingi,alisema Wenger.
Maandamano zaidi yanatarajiwa wakati wa mechi ya Jumamosi katika uwanja wa Emirates dhidi ya Norwich.

Trump achekwa kwa alivyotamka Tanzania

By on 12:47:00 PM
Trump alishambulia sana sera ya kigeni ya Obama


Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump amekejeliwa mtandaoni baada ya kuonekana akiboronga akitamka Tanzania wakati wa kutoa hotuba.
Bw Trump alikuwa akizungumzia mashambulio ya kigaidi yaliyotekelezwa katika mabalozi ya Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 wakati wa kuzungumzia sera yake ya kigeni.
Badala ya kutamka vyema ‘Tanzania’ anasikika akitamka ‘Tan-zay-nia’.
Mashambulio hayo yalitekelezwa na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda.
Msemaji wa ikulu ya White House pia alimcheka Bw Trump alipoulizwa kuhusu vile mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York alivyotamka jina Tanzania.
“Kweli, yamkini jinsi ya kutamka huwa haijaelezwa kwenye kifaa cha kuonesha maandishi ya hotuba,” alieleza afisa wa habari wa ikulu Bw Josh Earnest.

Magufuli: Polisi sharti wajirekebishe

By on 12:42:00 PM
Rais Magufuli amesema baadhi ya mambo yanachangia kuwepo kwa hali ngumu ya utendaji kazi Rais wa wa Tanzania Dkt John Magufuli amelitaka jeshi la polisi nchini pamoja na ofisi ya mwendesha mashitaka kujirekebisha katika utenda kazi na kujiepusha na kashfa.Amesema taarifa zinaonesha jeshi la polisi limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.Akiongea alipokuwa akifungua kikao cha kazi cha makamanda wa polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi, Dodoma ametoa mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya kununulia vifaa na sare za askari.Aidha, amezungumzia mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya polisi na wawekezaji akisema baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo.“Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa uwazi nitajisikia vibaya nikimaliza mkutano huu, nataka muelewe na muelewe ukweli direction (njia) ninayoitaka mimi.”Dkt. Magufuli pia amelitaka jeshi la polisi kujiepusha na kashfa ambazo zimekuwa zikisemwa dhidi yake, ikiwemo maafisa wa polisi kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kuazimisha silaha kwa wahalifu wa ujambazi.Kuhusu Ofisi ya Mwendesha Mashitaka, amesema amekuwa akisikitishwa sana na vitendo vya serikali kushindwa katika kesi nyingi mahakamani licha ya kuwa na wanasheria mahiri."Niwaombe mawakili na polisi wanaohusika na upelelezi mtangulize maslahi ya nchi mbele, kwa sababu kumekuwa na usemi kwa baadhi ya wapelelezi na mawakili wachache, nasema wachache, panapokuwa na kesi inayohusiana na pesa pesa, wana misemo yao wanasema dili limepatikana,” amesema.“Na saa nyingine kesi inapopelekwa mahakamani wana-collude (wanakula njama) mawakili wa serikali na mawakili wanaomtetea mhalifu, na wanapo-collude (wanapokula njama pamoja) siku zote serikali inashindwa.”

Wednesday, April 27, 2016