Akiandika
kwenye Twitter, Bw Trump ametetea uamuzi wake ulioshangaza wengi wa
kumfuta kazi mkuu huyo wa Shirika la Uchunguzi wa Jinai Marekani (FBI).
Rais
huyo alimfuta kazi kutokana na jinsi alivyoshughulikia uchukuzi wa
barua pepe za aliyekuwa mpinzani wa Bw Trump Hillary Clinton.
Bw Comey alikuwa anaongoza uchunguzi wa FBI kuhusu uhusiano kati ya maafisa wa kampeni wa Trump na Urusi.
Kufutwa kazi kwake kumewashangaza wengi Washington na maafisa wa chama cha Democratic pia wameeleza kushangazwa na uamuzi huo.
Kufutwa
kwake "kumeibua maswali kuhusu iwapo ikulu ya White House inaingilia
wazi uchunguzi wa jinai," alisema Adam Schiff, ambaye ni mwanachama wa
ngazi ya juu zaidi kutoka chama cha Democratic katika kamati ya bunge
kuhusu ujasusi.
Lakini kiongozi huyo ametetea uamuzi wake Jumatano asubuhi, saa chache kabla ya kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov - mkutano wa kwanza kati ya Trump na maafisa wa Urusi tangu achukue hatamu Januari.
0 comments:
Post a Comment