Tuesday, April 19, 2016

Machar afuta mpango wa kurejea Juba

By on 12:43:00 PM
https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=6465176323126612680#editor/target=post;postID=925816011096298285


Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa kiongozi wa waasi Riek Machar, amefutilia mbali mpango wake wa kurejea Juba kwa muda usiojulikana.
Msemaji wa serikali Michael Makuei amesema kuwa makamu wa bwana Machar, alitaka kurejea Juba na silaha nzito nzito, zikiwemo, magari ya kivita, makombora na bunduki nzito nzito.
Aidha amesema kuwa serikali ya nchi hiyo tayari imeruhusu wanajeshi elfu moja mia tatu na sabini kati ya elfu moja mia nne na kumi kurejea Juba kuja kumlinda Bwana Machar.
Amesema kuwa utawala wa nchi hiyo hautaruhsu wanajeshi zaidi kurejeshwa Juba, kutokana na sababu za kiusalama

Monday, April 18, 2016

Filamu nyingine ya Avatar kuongezwa

Filamu ya kwanza ya Avatar ilitolewa 2009 na iliwashirikisha Sam Worthington na Zoe Saldana

Watengenezaji wa filamu ya Avatar franchise wamesema kutatolewa filamu zaidi katika mwendelezo huo wa filamu, filamu ijayo ikitarajiwa kutolewa 2018.
Mwelekezi wa filamu hizo James Cameron ametangaza kwamba filamu hizo zitaendelezwa hadi makala ya tano itakayotolewa 2023.
Alikuwa tayari amethibitisha kwamba filamu tatu zaidi zingetolewa lakini amefichua kwamba kuna mambo mengi sana ya kuelezwa kwenye hadithi hiyo na makala zijazo tatu hazitoshi.

Kote duniani, Avatar inasalia kuwa filamu iliyofanikiwa zaidi katika historia.Filamu hiyo imezoa $2.7bn tangu kutolewa wake 2009.Filamu ijayo ya Avatar itatoka 2018, na hizo nyingine 2020, 2022 na 2023.

Boko Haram wavamia kambi ya jeshi Nigeria



Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wameishambulia kambi ya jeshi la Nigeria mapema asubuhi ya leo na kuua idadi kubwa ya wanajeshi huko Borno.

 .Mwanajeshi mmoja aliyeko Borno ameielezea BBC kuwa''wapiganaji wa Boko Haram waliwavizia na kuwashambulia alfajiri na mapema wakiwa wamelala.''''Wapiganaji hao walikuwa wamejihami kwa silaha kali na kusababisha maafa makubwa upande wa wanajeshi''
''Tuliwapoteza wenzetu wengi,,,,,wengi sana,, sijui hata ni wangapi waliojeruhiwa'' alisema mwanajeshi huyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake
Kambi hiyo ndogo iliyoko katika kijiji cha Kareto ilikuwa na wanajeshi wachache ambao kazi yao ilikuwa ni kulinda ngome kabla ya kikosi kikubwa zaidi kuwasili.
Hata hivyo mwanajeshi huyo anasema kuwa idadi ya wapiganaji hao ilikuwa kubwa mno hata wanajeshi kadhaa walitoroka ilikuokoa maisha yao.
''Walikuwa na silaha nzito nzito na kali kuliko zetu'' afisa huyo aliiambia idhaa ya BBC Hausa.
 
Mwanajeshi mmoja aliyeko Borno ameielezea BBC kuwa''wapiganaji wa Boko Haram waliwavizia na kuwashambulia alfajiri na mapema wakiwa wamelala.''
''Tuliwapoteza wenzetu wengi,,,,,wengi sana,, sijui hata ni wangapi waliojeruhiwa''
''Baadhi yetu walitoroka maji yalipozidi unga''
''Tuligundua idadi ya wavamizi ilikuwa ni kubwa kuliko yetu'' mwanajeshi mwengine aliiambia shirika la habari la AFP.
 
''Walikuwa na silaha nzito nzito na kali kuliko zetu'' afisa huyo aliiambia idhaa ya BBC Hausa.
Wapiganaji kadhaa waliuawa katika makabiliano hayo yaliyodumu kwa saa kadhaa kulingana na wenyeji wa kijiji hicho.
Hata hivyo jeshi lilijitahidi na kuikomboa kambi hiyo baada ya mashambulizi ya angani kuwasili na kuwaokoa wanajeshi walikuwa wamesakamwa ardhini.
Idadi kamili ya waliouawa haijajulikana.

Korea Kaskazini kulipua bomu la nyuklia

By on 10:09:00 AM
Korea Kaskazini ilifanyia majaribio bomu la haidrojeni Januari mwaka huu

Korea Kusini imesema imepata dalili kwamba Korea Kaskazini inajiandaa kufanya jaribio la tano la bomu la nyuklia, Rais Park Geun-hye amesema.
Hakufafanua zaidi kuhusu dalili hizo, lakini ameagiza jeshi la nchi yake kuwa tayari, shirika la habari la nchi hiyo limesema.
Kumekuwa na ripoti katika vyombo vya habari nchini Korea Kusini kwamba kumeongezeka shughuli katika kituo cha majaribio ya silaha za nyuklia cha Korea Kaskazini cha Punggye-ri, ambapo majaribio ya awali yalitekelezwa.
Iwapo Pyongyang itaendelea na kufanyia majaribio bomu la nyuklia, basi itakuwa ni kukaidi zaidi vikwazo vikali ilivyoongezewa na Umoja wa Mataifa mwezi jana.
"Tupo katika hali ya kutatanisha, hatujui iwapo Korea Kaskazini inaweza kufanya uchokozi kama njia ya kujitetea kutokana na kutengwa na jamii ya kimataifa na pia kuimarisha uungwaji mkono ndani ya nchi,” Bi Park aliambia maafisa wake wakuu wa jeshi, shirika la habari la Yonhap liliripoti
Mwezi Januari, Korea Kaskazini ilifanya jaribio la nne la silaha za nyuklia na baadaye ikarusha kombora baharini.
 
Kituo cha Punggye-ri
 
Hatua hiyo iliongeza hali ya wasiwasi katika rasi ya Korea.Waangalizi wanasema huenda jaribio hilo la bomu likafanywa kabla ya mkutano mkuu wa chama tawala cha Workers' Party mjini Pyongyang mwezi Mei.
Wataalamu wanaamini Korea Kaskazini haina uwezo wa kiteknolojia wa kuweka silaha ya nyuklia kwenye kombora, ingawa imepiga hatua kubwa katika mpango wake wa nyuklia miaka ya karibuni.

UN: Burundi inawatesa wapinzani wake

By on 10:03:00 AM
Idadi ya watu wanaoteswa nchini Burundi imeongezeka maradufu.


Idadi ya watu wanaoteswa nchini Burundi imeongezeka maradufu.
Umoja wa mataifa unasema kuwa katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza mwaka huu takriban watu 400 wameripotiwa kukamatwa na vyombo vya dola na kisha kuteswa..
Zeid Ra'ad Al Hussein anasema kuwa mawakala wake wamerekodi visa 345 za mateso na dhulma dhidi ya watu wanaokisiwa kuwa wapinzani nchini Burundi.

 
Mkuu wa kitengo cha haki za binadamu wa Umoja huo wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein anasema kuwa mawakala wake wamerekodi visa 345 za mateso na dhulma dhidi ya watu wanaokisiwa kuwa wapinzani nchini Burundi.
Tangu machafuko ya kisiasa yalipoanza mwaka mmoja uliopita, takriban watu 600 wameshikwqa na kuteswa na vyombo vya serikali ya rais Pierre Nkurunziza.
 
Add caMachafuko yalianza nchini Burundi rais Pierre Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kuwania muhula wake wa tatu . ption
''Hao ndio waliokuwa na shime ya kujitokeza ,tunashuku kuwa idadi ya wale walioteswa ni kubwa mno ila kutokana na hofu ya kukabiliwa na maafisa wa usalama wengi wanajificha'' alisema afisa huyo wa UN.
Wale wanaokamatwa na kuteswa mara nyingi wanasema kuwa wanapitia dhulma hiyo ndani ya vituo vya idara ya usalama wa taifa na kijasusi ya Burundi.
Hadi kufikia sasa takriban watu 400 wamethibitishwa kufariki

 
Machafuko yalianza nchini Burundi rais Pierre Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kuwania muhula wake wa tatu .
Rais Pierre Nkurunziza
 
 
Wapinzani wake walimkashifu kwa kukiuka katiba ya taifa huku rais mwenyewe akisisitiza kuwa wala hakukiuka kamwe katiba kwani muhula wa kwanza , alipoongoza taifa hilo hakuchaguliwa na umma bali wajumbe wa kamati maalum ya upatanisho iliyoundwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe 2005.
Hadi kufikia sasa takriban watu 400 wamethibitishwa kufariki huku zaidi ya watu laki mbili u nusu wakilazimika kutorokea mataifa jirani kwa hofu ya kuzuka mapigano mapya.

Saturday, April 16, 2016

Mkuu wa shirika la UN amshutumu Trump


Trump mwishoni mwa mwaka jana alipendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani


Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Haki za Kibinadamu ameshutumu sera za mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani, akisema ni sawa na ushenzi.
Zeid Raad al-Hussein, ingawa hakumtaja Bw Trump moja kwa moja, alizungumzia hatua ya mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York kuunga mkono mateso pamoja na sera zake kali dhidi ya Waislamu.
“Ushenzi na ulokole si thibitisho la uongozi thabiti,” Hussein alisema.
Kamishna huyo pia amekosoa mpango wa mgombea mwengine Ted Cruz wa kuweka mpango wa kupeleleza maeneo wanamoishi Waislamu.
“Kutoa matamshi ya chuki, kuchochea na kuwatenga wengine si jambo la kuburudisha watu nalo, au jambo la kujifaidi kisiasa,” Bw Hussein ameambia hadhira katika mji wa Cleveland, Ohio.

Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislam

 

 
Trump anaongoza kwenye kura za maoni miongoni mwa wagombea wa Republican
Vigogo wa chama cha Republican nchini Marekani wamemkemea mwenzao Donald Trump, anayetaka kuwania urais kupitia chama hicho, kwa kupendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.
Mmoja wa wanaoshindani tiketi ya kuwania urais Jeb Bush amesema Bw Trump "mwenye kasoro akilini”. Makamu wa rais wa zamani Dick Cheney naye alisema pendekezo hilo "linaenda kinyume na yote ambayo huwa tunatetea”.
Ikulu ya White House, Umoja wa Mataifa na viongozi wa Kiislamu pia wamekosoa matamshi hayo ya Trump.
Bw Trump alikuwa amesema Waislamu wengi wana "chuki” dhidi ya Marekani.
Kwenye hotuba wakati wa kampeni, aliomba "Waislamu wote wazuiwe kuingia Marekani hadi wawakilishi wa nchi wajue ni nini kinachoendelea”
Meneja wake wa kampeni alisema marfuku hiyo ingeathiri "kila mmoja” bila kubagua kama ni mhamiaji au mtalii.


Lakini Bw Trump aliambia Fox News kwamba haingeathiri “watu wanaoishi humu nchini (Marekani), akiongeza kuwa Waislamu wanaohudumu katika jeshi la Marekani wangekaribishwa "nyumbani”.
Matamshi hayo ya Bw Trump yalitolewa Marekani ikiendelea kuomboleza kufuatia shambulio mbaya zaidi la kigaidi kutekelezwa tangu shambulio la Septemba 11, 2001.
Wiki iliyopita, wanandoa wawili Waislamu, ambao wanaaminika kukumbatia itikadi kali, walifyatua risasi na kuwaua watu 14 na kuwajeruhi wengine 21 katika kituo cha afya San Bernardino, jimbo la California.
Bw Trump alishangiliwa sana aliporudia ahadi yake katika mkutano wa kampeni jimbo la South Carolina saa chache baada ya kutoa matamshi hayo mara ya kwanza.

Ameongeza: "Mmoja wa wagombea wanaoongoza katika kinyang’anyiro cha kutaka kuwa rais wa nchi hii alitangaza, miezi kadha iliyopita, kujitolea kwake kutumia mateso (…) kuumiza watu wengine, ili watoe habari au wabuni habari ambazo hawazo nazo.”
Bw Hussein amesema si vyema kukiuka haki za wengine kujifaa kisiasa
Wakati wa kampeni, bw Trump alisema kwamba mateso wakati mwingine hufanikiwa na akaahidi kurejesha njia hatari zaidi kuliko kutumia maji kulazimisha washukiwa kufichua habari.
Njia hizo zilitumiwa na jeshi la Marekani katika washukiwa wa ugaidi lakini zilipigwa marufuku na utawala wa Bw Obama.



Tetemeko la pili laikumba Kumamoto, Japan

By on 12:49:00 AM
Tetemeko hilo lilisababisha kuporomoka kwa majengo

Maafisa nchini Japan wanasema kuwa tetemeko kubwa la ardhi limewaua takriban watu 19 na kusababisha uharibifu mkubwa.
Tatemeko hilo ambalo ni la pili kukumba kisiwa cha Kyushu ndani ya siku mbili, limesababisha kuporomoka kwa majengo, limeharibu barabara pamoja na mifumo ya maji na umeme.
Tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 7.3 kwenye vipimo vya Richter.
Tetemeko hilo la ardhi, ambalo chanzo chake ni kilomita 10 chini ya ardhi karibu na mji wa Kumamoto, lilikuwa kubwa na liliathiri eneo kubwa kuliko la kwanza lililotokea katika mji huo wa Kumamoto Alhamisi usiku.
Watu wengi wamejeruhiwa
Afisa wa serikali wa Kumamoto Tomoyuki Tanaka ameambia AP kwamba idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.
Wanajeshi 20,000 wametumwa kusaidia juhudi za uokoaji lakini jitihada za uokoaji zimetatizwa na mitetemeko mingine midogomidogo.
Waziri mkuu Shinzo Abe amekuwa na mipango ya kuzuru ki