Friday, May 13, 2016

Mwanamke wa Senegal ateuliwa katibu mkuu Fifa


Samoura
Add caption

Ni mara ya kwanza mwanamke kuteuliwa katibu mkuu Fifa
Kwa mara ya kwanza katika historia, mwanamke ameteuliwa kuwa katibu mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), shirikisho ambalo kwa kiwango kikubwa limetawaliwa na wanaume.
Bi Fatma Samba Diouf Samoura kutoka Senegal, ndiye katibu mkuu mpya.
Atasimamia shughuli za kila siku katika shirikisho hilo ambalo kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa limekabiliwa na tuhuma za ulaji rushwa.
Ni mwanadiplomasia aliyehitimu ambaye kwa sasa amekuwa akihudumu kama mratibu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa nchini Nigeria.
Amefanya kazi UN kwa miaka 21.
Bi Samoura amesema ni fahari kubwa sana kwake kuteuliwa kwenye wadhifa huo.
Tangazo hilo limefanywa na rais wa FIFA Gianna Infantino katika kongamano kuu la FIFA linaloendelea Mexico.
Aliyekuwa katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke alipigwa marufuku kutojihusisha na shughuli zozote za soka kwa miaka 12 mapema mwaka huu.



















Mwanamume 'adandia' helikopta Bungoma Kenya

By on 12:57:00 PM
Ndege
Ndege hiyo ilipaa na kuondoka naye
Mwanamume mmoja katika mji wa Bungoma, Magharibi mwa Kenya ameshangaza wengi baada ya kudandia helikopta ambayo imepaa na kuondoka naye.
Helikopta hiyo ilikuwa imesafirisha mwili wa mfanyabiashara mashuhuri Jacob Juma aliyeuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi wiki iliyopita, vyombo vya habari nchini Kenya vinasema.
Video zinazosambaa mtandaoni zinaonesha helikopta hiyo ikipaa juu angani kutoka uwanja wa Posta, mwanamume huyo akiwa amejishikilia kwenye vyuma vya helikopta hiyo.
Taarifa zinasema baadaye ndege imetua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Bungoma na mwanamume huyo akapelekwa hospitalini.
Kitambulisha mada #Bungoma kimeanza kuvuma kwenye Twitter nchini Kenya, watu wakijadili tukio hilo.
Wengi wameeleza kushangazwa kwao na wengine wanalifanyia mzaha.
Baadhi wanasema mwanamume huyo alisahau leo ilikuwa Ijumaa tarehe 13, ambayo kwa baadhi ni siku yenye kutokea mabaya.Wengine wanatumia majina ya filamu na hata nyimbo. Mfano wimbo wa 'I Believe I Can Fly', wake R Kelly na filamu ya Mission: Impossible ambayo mwigizaji nyota wake ni Tom Cruise.https://www.blogger.com/blogger.g?blogID=6465176323126612680#editor/target=post;postID=2149767923202216375

Monday, May 9, 2016

Malkia wa Pembe' afikishwa kortini Tanzania

By on 12:31:00 PM



Malkia wa Pembe kutoka China Kesi dhidi ya mwanamke mfanyabiashara raia wa China anayetuhumiwa na mashtaka ya kuendeleza mtandaoa wa kihalifu wa ulanguzi wa pembe barani Asia imeahirishwa kwa wiki mbili nchini Tanzania.
Alifikishwa mahakamani Jumatatu asubuhi mjini Dar es Salaam.
Waendesha mashtaka wanasema Yang Feng Glan, anayejulikana kwa umaarufu pia kama Malkia wa pembe, aliendesha biashara haramu ya kuwaua ndovu katika mbuga za wanyama ili kupata pembe zao ambazo wanazisafirisha na kuziuza katika mataifa ya bara Asia.
Anashutumiwa kwa kuendeleza shughuli hiyo kwa takriban miaka 14.
Anakana mashtaka hayo.
Mahakama imeambiwa kwamba faili ya kesi yake bado imo mikononi mwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma.
Maafisa wa serikali Tanzania walitaja kukamatwa kwa Yang Feng Glan mnamo Oktoba mwaka jana kama ufanisi mkubwa.
Taifa hilo la Afrika mashariki limepoteza thuluthi mbili za ndovu wake katika kipindi cha miaka kumi iliyopita