Tuesday, November 17, 2015










                            Mechi 14 za kufuzu kwa kombe la dunia leo 


Mechi 14 za mkondo wa pili wa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia la mwaka wa 2018 nchini Urusi zinachezwa leo kote barani Afrika
Washindi katika mechi hizi ndio watakaofuzu kwa mkondo ujao na kujiunga na Uganda ambao tayari walijikatia tikiti baada ya kushinda Togo kwa jumla ya mabao 4-0.
Uganda, DR Congo, Morocco, Guinea na Gabon zilifuzu kusonga mbele katika hatua ya makundi baada ya kushinda mechi zao.
Gabon nao wakasonga mbele katika hatua ya makundi kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Msumbiji.
Nao Zambia, wakawachapa Sudan kwa 2-0 na kufuzu kwa makundi kwa jumla ya mabao 3-0 .
DR Congo walitoka sare ya 2-2 na Burundi huko kwao lakini wamesonga mbele baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-2 huko Bujumbura.
Morocco nao wamefuzu licha ya kufungwa 1-0 jana na Equatorial Guinea baada ya wao kushinda mechi ya kwanza 2-0.
Ratiba ya mechi za leo:
Rwanda v Libya 16:30 (0-1)
Cameroon v Niger 17:00 (3-0)
Ghana v Comoros 18:00 (0-0)
Nigeria v Swaziland 18:00 (0-0)
Congo v Ethiopia 18:00 (4-3)
Misri v Chad 19:30 (0-1)
Tunisia v Mauritania 20:00 (2-1)
Afrika Kusini v Angola 20:00 (3-1)
Ivory Coast v Liberia 20:00 (1-0)
Burkina Faso v Benin 21:00 (1-2)
Algeria v Tanzania 21:15 (2-2)
Mali v Botswana 22:00 (1-2)
Cape Verde v Kenya 22:00 (0-1)
Senegal v Madagascar 22:00 (2-2)

0 comments: