Job Ole Ndugai ndie spika mpya wa
bunge la Tanzania. Ndugai mwenye umri wa miaka 55 alijipatia thuluthi
mbili ya kura zinazohitajika.
Alikuwa naibu wa spika wa bunge lililokamilika.
Ndugai
anatarajiwa kuliongoza bunge lenye zaidi ya wabunge 100 kutoka upinzani
,ikiwa ndio idadi kubwa zaidi kuwahi kuchaguliwa katika bunge hilo.
Kulikuwa
na wagombea 8 waliowania wadhfa huo wa spika,lakini mwishowe ushindani
ulikuwa kati ya mgombea wa chama tawala cha CCM Job Ole Ndugai na
mwenzake wa upinzani Goodluck Ole Medeye kutoka chama cha Chadema.
Bunge
jipya litakuwa na wanachama 394,ikiwa linawawakalishi 30 zaidi
ikilinganishwa na bunge lililopita kufuatia kubuniwa kwa maeneo mapya ya
ubunge.
0 comments:
Post a Comment