Friday, November 20, 2015

Mali: Miili ya watu 18 imedaiwa kupatikana hotelini

                          Polisi wa Mali wameingia katika hoteli hiyo

Maafisa wa serikali ya Mali wamesema sasa hakuna mateka wowote waliosalia katika hoteli ya Radisson Blu mjini Bamako iliyokuwa imeshambulia asubuhi na watu wenye silaha huku miili ya watu 18 ikidaiwa kupatikana ndani ya hoteli hiyo.
Waziri wa usalama wa Mali Salif Traore ameambia kikao cha wanahabari kwamba watu wenye silaha walioshambulia hoteli ya Radisson kwa sasa hawazuilii mateka wowote.
Afisi ya rais wa Mali imeandika kwenye Twitter ikishukuru maafisa wa usalama na mataifa yaliyosaidia kukabiliana na shambulio hoteli hiyo ya kifahari.
Watu watatu wamethibitishwa kufariki na wanajeshi wawili kujeruhiwa.
Ubelgiji imesema afisa mmoja wa serikali yake ni miongoni mwa waliouawa kwenye shambulio hilo.
Geoffrey Dieudonne alikuwa Mali kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa serikali.
Uvamizi huo wa wanamgambo hao ulitekelezwa mapema asubuhi kwenye hoteli hiyo ya kifahari ambayo hupendwa sana na raia wa mataifa ya nje.

0 comments: