Friday, November 20, 2015

Facebook yaonywa ikome kudukua Ubelgiji

Mahakama moja nchini Ubelgiji imeipa Facebook saa 48 kukoma kuwadukua watu ambao hawajajiunga na mtandao huo wa kijamii.
Facebook imesema kuwa itakata rufaa uamuzi huo.
Kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii inadai kuwa mahakama hiyo imetoa kauli hiyo kwa sababu ya programu ambayo imekuwa ikiitumia nchini humo kwa kipindi cha miaka 5 sasa.
Programmu hiyo inajipachika kwa simu ya mtu aliyeingia kwenye mtandao huo wa Facebook pale hata kama sio hajajiunga na mtandao huo wa kijamii.
Hata hivyo mahakama hiyo Ubelgiji imesema uwa Facebook haina ruhusa ya kuwadakua watu ambao sio watumizi wa mtandao wake.
Na kama watataka kuwadukua, sharti wapate idhini ya mahakama.
Image copyright PA
Image caption Iwapo Facebook itakataa kutii amri hiyo itatozwa faini ya Euro 250,000 kwa siku.
''Mahakama imeamua kuwa habari za kibinafsi zinazokusanywa na Facebook ni kinyume cha sheria na hivyo lazima Facebook iwaombe ruhusa watumizi wake ilikuafikiana na sheria za Ubelgiji,'' taarifa hiyo ilisema.
Iwapo Facebook itakataa kutii amri hiyo itatozwa faini ya Euro 250,000 kwa siku.
Programu hiyo aina ya Cookies inapigamsasa mtumiaji wa Facebook ilikubaini kama yeye ama mashine anayoitumia imewahi kutumika kujiunga na mtandao huo wa Facebook.
Msemaji wa Facebook alisema kuwa wamekuwa wakitumia programu hiyo ya Datr kwa zaidi ya miaka 5 na hiyo ndio imekuwa ikisaidia kuhakikisha akaunti za watu bilioni moja u nusu iko salama.

0 comments: