Monday, May 9, 2016

Jumba la ghorofa laporomoka Mombasa

By on 12:17:00 PM

Maafisa wa serikali wamefika eneo hilo
Sehemu ya jumba kubwa la kibiashara mjini Mombasa imeporomoka siku chache baada ya jumba la makazi kuporomoka jijini Nairobi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.
Sehemu ya jumba hilo la Nyali Centre, yenye ghorofa sita, iliporomoka usiku wa kuamkia Jumatatu.
Hakuna aliyeripotiwa kujeruhiwa wakati wa mkasa huo.
Jumba la Nyali Centre huwa na kituo cha mazoezi na mgahawa maarufu.
Waziri wa serikali ya jimbo la Mombasa Francis Thoya amesema jumba hilo litachunguzwa kubaini iwapo ni thabiti.
“Nadhani sehemu ambapo vyoo hivyo vilifaa kuuunganishwa na jumba lenyewe ndiyo ilikuwa na shida. Ninamsaka mhandisi na aliyepewa kandarasi,” amesema.
“Lakini unapopata visa kama hivi, ni ishara tosha kuwa inafaa tuchunguze upya mijengo yetu. Kwa hivyo kutakuwa na ukaguzi wa baadhi ya mijengo mikuu ambayo inatumiwa na umma.”

Magufuli aahidi sukari ya bei ya chini

By on 12:09:00 AM

Serikali ya Tanzania imeagiza sukari ilikukabiliana na upungufu wa sukari uliopo nchini.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema badala ya kuwapa wafanyabiashara leseni ya kuagiza sukari kutoka ng'ambo serikali yenyewe ndio itaagiza sukari hiyo moja kwa moja.
Kauli hiyo inawadia baada ya mabohari zaidi kugunduliwa kote nchini yakiwa yamejaa sukari iliyoagizwa kutoka nje na ile iliyonunuliwa kwa wingi kutoka kwenye kampuni za kusaga sukari za humohumo Tanzania.
''Kuna mmoja ambaye amepatikana Arusha amehodhi zaidi ya tani elfu tano ya sukari naye mwengine huko Kilombero amenunua sukari yote kutoka kwa kampuni za humu humu nchini na akaficha.''
''Lakini hili ni swala la sasa tu, katika siku zijazo sukari itapatikana kwa wingi hapa Tanzania.Serikali imekwisha agiza sukari lakini hatutawapa hawa waliofilisi watanzania leseni ya kuingiza tena sukari.
''Serikali imeagiza na itauza sukari hiyo kwa bei ya chini... hilo ndilo lengo la serikali '' alisema rais Magufuli huku mawananchi wakimshangilia
Katika siku zijazo sukari itapatikana kwa wingi hapa Tanzania.Serikali imekwisha agiza sukari lakini hatutawapa hawa waliofilisi watanzania leseni ya kuingiza tena sukari.''
.
 ''
Sukari hiyo ambayo huwa ni ya bei ya chini hubadilishwa na kisha kuvikwa magunia ya makampuni ya Kitanzania yanayosaga sukari na kisha kuuzwa rejareja.
Tumbua tumbua ya rais Magufuli imesadifiana na tangazo la Halmashauri ya ushuru ya Tanzania TRA kuwa imeanza kugawa sukari iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria na kufichwa katika mabohari kote nchini.
TRA ilichukua hatua hiyo baada ya mwekezaji wa kibinafsi mkoani Lindi kupatikana na zaidi ya mifuko elfu tano za sukari kutoka nga'mbo.
Yamkini sukari hiyo hubadilishwa kwenye mifuko yenye nembo ya kampuni za kusaga sukari za Tanzania na kisha kuuzwa kwa bei maradufu.

Saturday, May 7, 2016

Naibu kamanda wa kundi la mauaji Rwanda akamatwa

  • Saa moja iliyopita
Image copyright
Image caption Mpiganaji wa kundi la FDLR
Wakuu wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wanasema wamemkamata naibu kamanda wa kundi la wapiganaji, linalohusishwa na mauaji makubwa ya Rwanda ya mwaka 1994.
Msemaji wa serikali, alieleza kuwa Jenerali Leopold Mujyambere, wa kundi la Rwanda la FDLR, alikamatwa mjini Goma, mashariki mwa nchi.
FDLR kisangani
 
Kundi la FDLR ni la Wahutu wanaoshutumiwa kuuwa malaki ya Watutsi na Wahutu waliokuwa na msimamo wa wastani, wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Rwanda imeingilia kati kijeshi mashariki mwa Congo katika juhudi za kuliangamiza kundi hilo.

downlod

DIRA YA DUNIA JUMATATU 02.05.2016

dira ya dunia

downlod