Tuesday, March 29, 2016

Wa-Mexico wachoma mfano wa 'Trump'


Wa-Mexico wachoma mfano wa 'Trump'
Raia wa Mexico wanaosherehea sikukuu ya pasaka wamekuwa wakichoma sanamu za mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha Republicans Donald Trump.
Mojawapo ya tukio hilo la kushangaza limefanyika katika kitongoji kimoja cha wakaazi walio na kipato cha chini kiitwacho La Merced.
Wakaazi wengi wa La Merced wamejitokeza kushuhudia kuchomwa kwa kikaragosi cha Trump badala ya kile cha yule mfuasi wa Yesu Kristu aliyemsalito Judas Iscariot.
Wamexico wengi hawampendi bw Trump tangu alipotoa matamshi ya kuwakejeli wamexico.

Wamexico wengi hawampendi bw Trump tangu alipotoa matamshi ya kuwakejeli wamexico.
Desturi hiyo ya kuchoma vikaragosi hutumiwa na wamexico kuelezea hisia zao dhidi ya wanasiasa wenye sera wasizozipenda wakitolea mfano wa jinsi Judas Iscariot, alivyomsaliti Yesu.




Marekani yaifungua iPhone ya Mlipuaji

Wizara ya Sheria ya Marekani inasema imefanikiwa kuzisoma data zilizohifadhiwa kwenye Simu ya iPhone mali ya mmoja wa walipuaji katika tukio la mauaji la San Bernardino na kutangaza kuacha mpango wake wa kisheria dhidi ya Kampuni ya Apple.
Wakili wa Marekani Eileen Decker alisema kuna mtu aliisaidia idara hiyo kuifungua Simu hiyo ya iPhone bila kuathiri data zilizohifadhiwa.
Kampuni ya Apple ilikataa kusaidia uchunguzi , kwa kusema ni kuweka ' historia mbaya.
Simu hiyo ni mali ya Rizwan Farook ambaye, pamoja na mke wake, waliuua watu kumi na wanne kusini mwa California Desemba mwaka jana.

Milio ya risasi jengo la Bunge Marekani

Kuna taarifa za milio ya risasi katika viunga vya jengo la Makao Makuu ya Bunge la Congress, US Capitol Hill.
Mashuhuda wanasema wameambiwa kwa vipaza sauti kuwa kila mtu ajifiche.
Taarifa za hivi punde zinasema mtu huyo mwenye silaha amekamatwa na polisi mmoja amepigwa risasi na kujeruhiwa.
Waandishi wa Habari waliokuwa kwenye eneo jengo la Bunge wameambiwa waendelea kubaki ndani.
Ikulu ya White House nayo imefungwa. Msemaji wa Polisi katika Jengo la Bunge hajasema lolote lakini ameahidi polisi kutoa taarifa za tukio hilo wakati wowote.

Ndege ya Misri iliotekwa nyara yatua Cyprus

By on 12:57:00 AM

Ndege iliotekwa nyara imetua katika uwanja wa ndege wa Larnaca nchini Cyprus.
Duru za ndege hiyo pamoja na zile za serikali ya Misri zimenukuliwa zikisema ndege hiyo ya abiria iliokuwa ikisafiri kutoka mjini Alexandria kuelekea Cairo ilitekwa nyara na watu waliojihami.
Waliiamrisha ndege hiyo kutua Cyprus, msemaji wa shirika la ndege la AirMisri alinukuliwa akisema.
Shrika la habari la Cyprus limeripoti kwamba watu 55 wamo ndani ya ndege hiyo.
Kulikuwa na ripoti za awali kwamba zaidi ya watu 80 wamo ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo aina ya MS181,airbus A320 ilibeba abiria 81.
Abiria aliyedaiwa kuwa alikuwa amevaa ukanda wa mlipuaji wa kujitolea mhanga aliagiza rubani kuelekea Cyprus kulingana na AgyptAir.
Maafisa wa polisi wa Cyprus wamesema kuwa wale walioiteka hawakuitisha chochote ilipotua.
Uwanja wa ndege wa Larnaca umefungwa huku ndege zilizosubiriwa kutua zikielekezwa kwengineko.

Friday, March 25, 2016

Kiongozi wa IS auwawa Syria

Abdul Rahman Mustafa al-Qadul
Kiongozi wa pili kwa ukubwa katika itifaki ya kundi la wapiganaji la Islamic State ameuawa katika oparesheni iliotekelezwa na Marekani nchini Syria mwezi huu, vyombo vya habari vya Marekani vimesema.
Maafisa wa ulinzi wameliambia shirika la habari la NBC kwamba Abdul Rahman Mustafa al- Qaduli,raia wa Iraq anayejulikana kama Hajji Iman aliuwawa katika uvamizi mwezi huu.
Waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani Ash Carter alitarajiwa kuthibitisha kifo cha mwana jihad huyo na kutoa maelezo ya uvamizi huo.
Marekani ilikuwa imetoa zawadi ya dola milioni saba kwa mtu yeyote ambaye angetoa habari za Qaduli.
Qaduli alizaliwa mwaka 1957 ama 1959 kaskazini mwa mji wa Iraq wa Mosul ambao ulidhibitiwa na IS tangu mwaka 2014.
Alijiunga na al-Qaeda nchini Iraq mwaka 2004 chini ya uongozi wa marehemu Abu Musab al-Zarqawi akihudumu kama naibu wake na kiongozi wa eneo la Mosul kulingana na Marekani.
Baada ya kuachiliwa kutoka kwa jela za Iraq mapema mwaka 2012,alijiunga na vikosi vya IS nchini Syria.

Thursday, March 24, 2016

Wakuu wa mitihani Kenya wafutwa kazi


Waziri Nkaissery amesema watakaopatikana na hatia wataadhibiwa

Serikali ya Kenya imewafuta kazi maafisa wakuu wa Baraza la Mitihani Kenya (KNEC) kutokana na visa vya udanganyifu vilivyoripotiwa wakati wa mitihani ya kitaifa mwaka jana.Waliofutwa kazi ni pamoja na afisa mkuu mtendaji wa baraza hilo Bw Joseph Kivilu na mwenyekiti wa bodi inayosimamia baraza hilo Bw Kibiru Kinyanjui.Bw Kivilu pamoja na maafisa wengine saba wa baraza hilo wametakiwa kuandikisha taarifa kwa polisi mara moja.Tangazo la kufutwa kwa wakuu hao limetolewa kwenye kikao cha wanahabari kilichoandaliwa na Waziri wa usalama na masuala ya ndani Meja Jenerali Joseph Nkaissery na Waziri wa Elimu Fred Matiang’i.


Bw Matiang'i

Bw Nkaissery amesema hatua zitachukuliwa dhidi ya waliohusika katika uadanganyifu huo.
Watahiniwa waliopatikana na makosa ya udanganyifu mtihani wa kidato cha nne mwaka 2015 waliongezeka asilimia 70 kutoka mwaka uliotangulia.
Katika mtihani wa mwaka 2015, watahiniwa 5,101 waligunduliwa kuwa walitumia udanganyifu katika mtihani.
Mwaka 2014, ni watahiniwa 2,975 pekee waliokuwa wametumia hila katika mtihani huo wakati huo visa vikiwa vimepungua kutoka visa 3,812 mwaka 2013.


Visa vya udanganyifu viliongezeka asilimia 70 mwaka 2015

Aliyekuwa naibu chansela wa chuo kikuu cha Nairobi Prof George Magoha ameteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa bodi hiyo na ataanza kufanya kazi mara moja.
Muda mfupi baada ya tangazo la kufutwa kwa wakuu hao kutolewa, Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakieleza hisia zao na kitambulisha mada #KNEC kimeanza kuvuma.

Monday, March 21, 2016

VID-20151207-WA0012.mp4

Tuesday, March 15, 2016

Trump ashinda majimbo muhimu Marekani

By on 11:40:00 PM

Mshindi chama cha Republican Florida na Ohio hukabidhiwa wajumbe wote

Donald Trump amepiga hatua katika kukaribia kutwaa tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani baada ya kushinda mchujo majimbo matatu makubwa, likiwemo jimbo la Florida.

Bilionea huyo kutoka New York ameshinda majimbo ya Illinois na North Carolina.

Hata hivyo ameshindwa na John Kasich jimbo la Ohio.

Mgombea anayeongoza chama cha Democratic Hillary Clinton naye amepanua uongozi wake kwa kupata ushindi majimbo ya Florida, Ohio, Illinois na North Carolina.

Marco Rubio, mmoja wa waliotarajiwa kutoa ushindani kwa Trump katika chama cha Republican amejiondoa baada ya kushindwa na Trump katika jimbo lake la nyumbani la Florida.

Majimbo matano makubwa, Florida, Missouri, North Carolina, Ohio, Missouri na Illinois, yalifanya mchujo Jumanne.

 

Trump amemsifu Rubio

  Lazima tuunganishe chama,” amesema Bw Trump akihutubu Palm Beach, Florida, baada ya kupata ushindi.

Anatumai kwamba ushindi huo utamfungulia njia ya kupeperusha bendera ya chama cha Republican.

John Kasich hata hivyo ameshinda jimbo lake la kwanza tangu mchujo kuanza, jimbo la Ohio ambako yeye ndiye gavana.

Akihutubu baada ya ushindi, Bw Kasich amesema anataka kuweka “mazingira ya kubuni nafasi” kwa vizazi vijavyo na pia akampongeza Bw Rubio kwa kampeni yake.

Bw Rubio ametangaza kujiondoa kwake kwenye kinyang’anyiro katika mkutano wa kampeni mjini Miami baada ya kushindwa Florida.

Amesema Marekani imo kwenye dhoruba ya kisiasa na kwamba wapiga kura wamekasirika na kutamauka.

 Clinton amemshutumu Trump akisema anawagawanya Wamarekani


Katika jiji hilo, Bi Clinton ametoa hotuba yake akifurahia ushindi ambapo amemshutumu Bw Trump na kusema „Wamarekani wana hamu ya kupata suluhu (kwa changamoto zinazowakabili)”.
Mpinzani wake, seneta wa Vermont Bernie Sanders, amewahakikishia wafuasi wake Phoenix, Arizona, kwamba atasalia kwenye kinyang’anyiro na kusema tayari kampeni yake imezidi matarajio ya wengi.
Majimbo ya Florida na Ohio huwa muhimu sana kwa chama cha Republican kwani mshindi hukabidhiwa wajumbe wote.
Florida huwa na wajumbe 99 na Ohio wajumbe 66.