Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.
Waziri
Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa
kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya
kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu ambayo
hakuyafurahia.
Maafisa
hao, ambao kwa sasa tunahifadhi majina ili Jeshi la Polisi liweze
kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri.
Hii
imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya
zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini
katika mtandao wa TRA hayaonekani.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa
akiagana na viongozi wa TRA na TPA.
0 comments:
Post a Comment