Tuesday, December 1, 2015

Utafiti:Ulaji wa miraa unapunguza nguvu za kiume

Ulaji wa Miraa unaathiri nguvu za kiume.
Utafiti uliofanywa kwa niaba ya serikali ya Kenya na wahadhiri wa chuo kikuu cha Moi kilichoko katika Bonde la ufa umebaini kuwa Majani ya miraa inayofahamika pia kama 'Mairungi' unazuia ukuaji wa manii.
Aidha ulaji wa kipindi kirefu wa miraa unafanya mbegu za kiume za wanaume kufa haraka pindi zinapowekwa kwenye uke.
Mtafiti mkuu wa chuo kikuu cha Moi, Ochiba Lukanda, anasema kuwa utafiti sawa na huo uliofanywa huko ghuba ulibaini matokeo kama hayo.
Lukanda anasema kuwa wanaume ambao wamekuwa wakila Miraa kwa kipindi kirefu na wakaacha huwa wanapata uwezo wao wa kutunga mimba.
Ulaji wa Miraa pia huwa unasababisha mshtuko wa moyo.
''Mtu anapokula mmea huu baada ya muda damu yake huaanza kwenda kwa kasi, mbali na shinikizo la damu mumea huu hausababishi saratani kama inavyodaiwa '' Dakta Lukanda

0 comments: